Serikali ya Uingereza imeidhinisha kununuliwa kwa klabu ya Chelsea kwa kima cha pauni nilioni 4 nukta 25, na kampuni ya mmimiliki mwenza wa kampuni ya LA Dodgers Todd Boehly.
Chelsea ilitangaza kuuzwa mwezi Machi wmaka huu kabla ya mmiliki Roman Abramovich kuwekewa vikwazo kutokana na uhusiano wake na karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Chelsea imekuwa ikiendeshwa chini ya leseni maalum ya serikali itakayokamilika Mei 31.
Serikali ya Uingereza imedinda kuwa Abramovicha hatapara hela zozote kutokana na uuzaji wa klabu hiyo ,badala yake zitawekwa katika akaunti yake iliyofungwa na kuelekezwa kwa miradi ya kusaidia jamii.