Serikali yajizatiti kuhakikisha inaafikia kiwango cha asilimia 10 ya misitu nchini

Huku Serikali ikijizatiti kuhakikisha taifa hili linaafikia asilimia 10 ya kiwango cha msitu nchini, Chuo cha mafunzo kwa maafisa wa Magereza huko Ruiru kimetoa miche 997,400 za miti kwa upanzi wakati huu wa msimu wa mvua.

Also Read
Polisi wamkamata mmiliki wa shamba la bangi katika eneo la Soy

Hatua hiyo imeafikiwa chini ya mpango wa serikali wa kupanda miti bilioni 1.8 kwa lengo la kuafikia asilimia 10 ya eneo la misitu nchini ifikiapo mwaka wa 2022.

Chini ya mpango huo serikali inapania kupanda miti milioni mbili ya kiasili, na alfu 150 ya matunda kama vile Avacado au parachichi, maembe na mikandamia.

Also Read
Mbunge wa Emurua Dikir Johana Ngéno kusalia korokoroni hadi Alhamisi

Inspekta Boniface Kaloki kutoka chuo hicho cha maafisa wa magereza, alisema kufikia sasa wamepanda miti katika eneo la ekari 2,471, kwa ushirikiano na huduma ya vijana kwa taifa.

Also Read
Serikali yajizatiti kushughulikia ukosefu wa ajira nchini

Awamu ya pili inalenga kutoa miche milioni mbili chini ya mpango unaofadhiliwa na serikali kwa ushirikiano na benki ya Kenya commercial na wahisani wengine.

  

Latest posts

Jimmy Wanjigi afikishwa Mahakamani

Tom Mathinji

Wataalam wa uchunguzi wapelekwa katika mto Yala

Tom Mathinji

Mwanafunzi akufa maji katika bwawa kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi