Serikali yaondoa ushuru unaotozwa mahindi yanayoagizwa humu nchini

Ni afueni kwa wakenya huku bei ya unga wa mahindi ikitarajiwa kupungua, baada ya serikali kuondolea mbali malipo yote na ushuru unaotozwa mahindi yanayoagizwa humu nchini.

Akiongea katika kituo cha mpakani cha Namanga, waziri wa kilimo Peter Munya alisema hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na bei ya juu ya unga wa mahindi, ambayo imeathiri familia nyingi hapa nchini

Also Read
Mudavadi ajitosa rasmi ulingoni huku mwangwi wa BBI ukivuma kote nchini

“Hatua hii inalenga kupunguza gharama ya unga wa mahindi na chakula cha mifugo hapa nchini kwa muda wa siku 90, kabla ya kuanza kwa msimu wa upanzi,”alisema waziri Munya.

Waziri Munya aliserma serikali iliafikia uamuzi huo baada ya mashauriano ya kina na wadau wakuu baada ya taifa hili kuendelea kushuhudia upungufu mkubwa wa mahindi.

Also Read
Hasara yawakodolea macho wakulima wa Meru kutokana na uvamizi wa nzige

Munya alisema hatua hiyo inakusudiwa kuwawezesha waagizaji wa kibinafsi wa mahindi, kuagiza mahindi ya kutosha humu nchini na kupunguza gharama ya usagaji unga wa mahindi.

Waziri Munya hata hivyo amewaonya wakulima walaghai wanaoficha mahindi ili kusababisha uhaba bandia akisema hivi karibuni bei hiyo itapungua na akawatahadharisha wajiandae kupata hasara.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia mzozo katika kituo cha mpakani cha Namanga ambako zaidi ya malori 200 yanayosafirisha mahindi humu nchini yamekwama kwasababu ya ushuru wa juu.

Also Read
Lee Kinyanjui Apinga Matokeo ya Ugavana Nakuru

Waziri alisema tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa hatua hiyo ni tarehe mosi mwezi Julai na itakelezwa kwa siku 90.  Kwa sasa mfuko wa kilo mbili wa unga wa mahindi unauzwa kati ya shilingi 200 na shilingi 220.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi