Serikali yapiga marufuku uagizaji kibinafsi wa chanjo dhidi ya Covid-19

Serikali imepiga marufuku mara moja uagizaji wa kibinafsi,uuzaji na matumizi ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 hadi itakapohakikisha kuna uwazi na uwajibikaji katika utaratibu wa kuagiza chanjo hizo.

Hatua hiyo inatokana na hisia mseto kufuatia hatua ya kampuni moja ya kibinafsi nchini kuagiza chanjo ya Sputnik V iliyozinduliwa nchini Russia.

Also Read
Wahudumu wa afya watakiwa kuripoti visa vipya vya Saratani

Kuweko kwa chanjo hiyo nchini, kulibainika juma hili baada ya naibu Rais Dkt.William Ruto,mkewe Rachel pamoja na mawakili wawili wa hapa Nairobi kuchapisha picha mitandaoni wakiwa wanapokea chanjo hiyo.

Akihutubia wanahabari,waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema hakuna leseni itakayotolewa kwa kampuni za kibinafsi kuagiza chanjo ya Covid 19, huku ikifutilia mbali leseni ambazo tayari zilikuwa zimetolewa.

Also Read
Afrika Kusini yatangaza masharti mapya ya kudhibiti Covid-19

Waziri alisisitiza kwamba serikali pekee ndiyo itakayoagiza chanjo hizo.

Kagwe aliongeza kwamba yoyote atakayepatikana akitoa chanjo ya kukabiliana na corona kwa malipo,atakuwa akikiuka sheria na hivyo basi ataweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Also Read
Viongozi wa Migori waagizwa kuhamasisha wanafunzi wote kurejea shuleni

Wakati huo huo,waziri wa afya amehimiza serikali za kaunti kuimarisha kampeini ya kutoa chanjo.

Kaunti pia zimetakiwa kutumia mgao wote wa dozi zao za chanjo ya corona huku shehena ya pili ya chanjo hiyo ikitarajiwa nchini wakati wowote.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi