Serikali yapunguza gharama ya pembejeo za kahawa

Serikali imezindua mpango utakaowezesha wakulima wa kahawa kununua pembejeo za zao hilo kwa gharama nafuu katika Kiambu, kwa kuondolewa asilimia 40 ya bei za pembejeo hizo.

Mpango huo unaotekelezwa na muungano wa vyama vya ushirika wa New Kenya Planters Corporative Union (New KPCU), utawapiga jeki wakulima wa mbuni wa vyama vya ushirika na vile vile wakulima wa mashamba madogo-madogo, ambapo watapewa kadi za utambulisho wanaponunua pembejeo hizo kama vile mbolea na dawa za kuua wadudu waharibifu,kutoka kwa wasambazaji walioidhinishwa kwa bei nafuu.

Also Read
Uhuru Kenyatta: Wasioridhika serikalini wajiuzulu
Also Read
KUPPET yapinga kozi za lazima za kutoa mafunzo kwa walimu

Akihutubia wakulima katika uwanja wa Ndumberi,kaunti ya Kiambu, waziri wa kilimo Peter Munya,alisema hatua hiyo itawafaidi wakulima hao kupata pembejeo nyingi kutoka kwa wasambazaji walio karibu nao.

Also Read
Rais Kenyatta afungua rasmi barabara mpya

Hata hivyo,Munya, alitishia kuvunja kamati za vyama vya ushirika ambazo hazitatia sahihi fomu za maombi ya malipo ya mapema ya mbuni kati ya kipindi cha majuma mawili.

  

Latest posts

Mtangazaji mkongwe Khamisi Themor kuzikwa siku ya Ijumaa

Tom Mathinji

NPS: Oparesheni ya kiusalama Turkana yazaa matunda

Tom Mathinji

Bodi ya dawa na sumu yapiga marufuku uuzaji wa dawa ya kupanga uzazi ya ‘Sophia’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi