Serikali yasitisha kubuni maeneo mapya ya kiutawala

Na Ripota Wetu.

Serikali imesimamisha uanzilishi wa maeneo mapya ya kiutawala na ugavi wa ardhi kwenye mpaka wa kaunti za Isiolo na Meru hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Marufuku hayo yalitangazwa siku ya Jumanne na waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i wakati wa mkutano ulioandaliwa katika hoteli moja ya Isiolo.

Also Read
Serikali kuratibu sheria kuwazuia polisi kujihusisha kimapenzi baina yao
Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai.

Matiang’i ambaye aliongoza mkutano wa amani katika kaunti hiyo alisema kutokana na kuingizwa kwa siasa katika mipaka ya utawala, marufuku hayo yatatoa muda wa kutosha wa kushirkisha umma na kuzuia mizozo zaidi katika sehemu hiyo hasaa wakati huu wa uchaguzi.

Also Read
Machifu watakaochangia kuficha visa vya mimba za mapema kufutwa kazi
Mkutano wa kiusalama ulioongozwa na waziri wa usalama Dkt Fred Matiang’i katika kaunti ya Isiolo.

Mkutano wa pamoja na makundi ya maafisa wa usalama kutoka kaunti za Isiolo na Meru, pia ulijadilia kuhusu hatua za kugawana raslimali ili kukomesha ghasia za mara kwa mara kwenye mpaka wa kaunti hizo mbili zinazotokana na tatizo la ukame.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi