Serikali yatakiwa kuimarisha usalama katika mpaka wa kaunti za Laikipia na Isiolo

Wakazi wa eneo la mpaka kati ya kaunti za Laikipia na Isiolo wamehimiza serikali kuimarisha usalama katika sehemu hiyo kufuatia mauaji ya watu sita.

Akiongea katika hafla ya mazishi ya  James Ntinai aliyekuwa na umri wa miaka 39,ambaye aliuawa na wahalifu, mbunge wa Laikipia kaskazini Sarah Lekorere alitoa wito kwa serikali kudumisha usalama katika sehemu hiyo.

Also Read
Barabara ya Isiolo-Moyale yatajwa kuwa kitovu cha usafirishaji mihadarati

Mbunge huyo alisema wakazi wengi sasa wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na wahalifu.

Wakazi hao sasa wamedai  maafisa wa usalama wamezembea katika majukumu yao na sasa visa vya uhalifu vimekithiri katika sehemu hiyo.

Hayo yanajiri  wiki moja baada ya kamishna wa eneo la Rift Valley  George Natembeya kuzuru sehemu hiyo na kutoa wito kwa jamii za sehemu hiyo kuishi kwa amani.

Also Read
Jamii ya Turkana yalalamikia kudhulumiwa na maafisa wa Polisi

Aliyekuwa wakati mmoja mwenyekiti wa tume ya mshikamano wa kitaifa Francis Kaparo alisema watu wanaowavamia wakazi wamekuwa wakidai kwamba wakazi wamedinda kuunga mkono ari yao ya kuvamia mashamba makubwa kwa ajili ya leshe kwa mifugo wao.

Also Read
Washukiwa wawili wa ugaidi wakamatwa Mjini Mombasa

Kaparo alitoa wito kwa serikali kuwapeleka maafisa wa kutosha wa usalama katika sehemu hiyo kuwalinda wakazi wanaohofia kushambuliwa.

Kulingana na Kaparo tayari baadhi ya wakazi hao wameanza kuhama makwao na kukimbilia usalama katika kituo cha biashara cha Kimanjo.

 

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi