Serikali yatetea hatua ya kufunga barabara ya Thika jana usiku

Waendeshaji magari jijini Nairobi jana usiku walikwama wakati polisi walipoweka vizuizi kwenye barabara muhimu wakati wa kafyuu.

Waendeshaji magari walikwama kwenye barabara ya Thika kwa saa kadhaa huku baadhi yao wakiwalaumu polisi kwa kuweka vizuizi barabarani.

Jijini Nairobi na katika maeneo mengine yaliyoathiriwa muda wa kafyuu ni kati ya saa mbili usiku na saa kumi alfajiri.

Also Read
Etana Kutumbuiza Nairobi

Kufikia saa mbili usiku jana, waendeshaji magari wengi walikuwa wangali barabarani.

Baadhi ya waendeshaji magari walionekana wakipiga kelele ilhali wengine walikuwa wakipiga picha na kulalamika kupitia mitandao ya kijamii.

Lakini serikali imetetea hatua yake, ikisema kwamba Wakenya wote sharti wazingatie kanuni zilizowekwa.

Also Read
Watu 184 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Hatibu wa serikali, Cyrus Oguna, alisema ni muhimu kwa watu kuendelea kuzingatia kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19 ili kudhibiti msambao wa ugonjwa huo na kurejelea maisha ya kawaida.

Polisi waliweka vizuizi barabarani kutekeleza agizo la muda wa kafyuu, hali iliyowaathiri mamia ya waendeshaji magari kwenye barabara kuu na barabara nyingine.

Also Read
Mwanajeshi wa zamani akamatwa na barua feki za usajili wa KDF

Muda wa kafyuu utaendelea kote nchini hadi tarehe 29 mwezi ujao.

Marufuku ya usafiri ilitangazwa katika kaunti tano tarehe 29 mwezi uliopita wakati Rais Uhuru Kenyatta alipopiga marufuku usafiri kuingia na kutoka katika eneo la kaunti hizo tano.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi