Serikali yawahamisha Makamishna wa Maeneo

Siku moja baada ya kujiuzulu kwa George Natembeya  wadhifa wa kamishna wa eneo la Rift Valley, katibu katika wizara ya usalama Dkt. Karanja Kibicho, ametangaza kuhamishwa kwa makamushna wa maeneo.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa kamishna wa kaunti ya Makueni Mohammed Maalim,ndiye kamishna mpya wa eneo la Rift Valley.

Also Read
Malkia Strikers kuondoka nchini Alhamisi kwa kambi ya Olimpiki mjini Kurume

Maalim anachukua mahala pa George Natembeya ambaye alijiuzulu Jumatano na kujitosa kwenye ulingo wa siasa ambapo atakuwa mgombeaji wa kiti cha ugavana cha Trans Nzoia katika uchaguzi mkuu ujao.

Natembeya sasa amerejeshwa katika ofisi ya Rais. Ofisi ya rais pia imemteua William Kang’ethe Thuku kuwa kamishna mpya wa eneo la Nairobi.

Also Read
Chama cha KUPPET chasema shule haziko tayari kufunguliwa

Kamishna wa eneo la Mashariki Isaiah Nakoru amehamishwa hadi eneo la magharibi kwa wadhifa huo huo na nafasi yake kuchukuliwa na kamishna wa kaunti ya Narok Evans Achoki ambaye amepandishwa cheo.

Kamishna wa eneo la magharibi Esther Maina, pia amehamishwa hadi eneo la kati huku mwenzake wa Nairobi James Kianda akipelekwa kuhudumu eneo la kaskazini Mashariki kuchukua nafasi ya Nicodemus Ndalana ambaye amerejeshwa katika jumba la Harambee.

Also Read
Taliban yateka gereza moja na kuwaachilia huru wafungwa

Kamishna wa eneo la kati Wilfred Nyangwanga, vilevile amrejeshwa katika jumba la Harambee.

  

Latest posts

ECOWAS kuiwekea Burkina Faso Vikwazo

Tom Mathinji

Rwanda kufungua mpaka baina yake na Uganda

Tom Mathinji

Waagizaji magari na pikipiki kutoka nje ya nchi kusajiliwa upya

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi