Sharlet Mariam ajitoa kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni

Mgombea huru Sharlet Mariam amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo katika Eneo Bunge la Msambweni utakaofanyika tarehe 15 mwezi Disemba, mwaka huu.

Akiwahutubia wanahabari, Mariam, ambaye alikuwa msaidizi wa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema sasa atamuunga mkono mwaniaji wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM Omari Boga.

Also Read
Kenya yanakili visa vipya 511 vya maambukizi ya Korona

Aliwaambia wanahabari kwamba alifanya uamuzi huo baada ya kukutana na wafuasi wake ambapo walikubaliana kwamba hakuna haja  ya kuufanya uchaguzi huo mdogo kusababisha mgawanyiko.

“Tunataka wanawake wetu hapa Msambweni wasiangamie. Vijana wetu wasiangamie na chama (cha ODM) kiko imara na hapa Msambweni wataona kivumbi,” akasema Mariam.

Also Read
Nderitu Muriithi: Nitatetea wadhifa wangu wa Ugavana kwa tiketi ya PNU

Baada ya kukihama chama cha ODM, Mariam alitaka kugombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Jubilee kabla chama hicho kutangaza kwamba hakitajihusisha kwenye kinyang’anyiro hicho.

Also Read
Maafisa wa polisi waliohusika na mauaji ya kaka wawili Embu kushtakiwa

Kufuatia tangazo hilo, Mariam alilazimika kuwa mgombea huru ambaye aliidhinishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC mwezi uliopita.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori mwezi Machi mwaka huu.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi