Sharon Jeptarus ameongeza nishani ya fedha kwa Kenya katika mbio za mita 1500 wanawake kwenye makala ya 24 ya michezo ya Olimpiki kwa walemavu wa kuskia inayoendelea mjini Caxius Do Sul nchini Brazil.
Jeptarus aliye na umri wa miaka 24 kutoka Eldoret,aliongoza mbio hizo kutoka mwanzo lakini akalemewa katika mzunguko wa mwisho na kumaliza wa pili kwa muda wa dakika 4 sekunde 49 nukta 98,nyuma ya Anastacia Sydorenko kutoka Ukraine aliyenyakua dhahabu kwa dakika 4 sekunde 49 nukta 31.
Mio Okada kutoka Japan alinyakua nishani ya shaba kwa ddakika 4 sekunde 52 nukta 78.

“Nafurahia kushinda nishani katika mara yangu ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa “akasema Jeptarus .
“Tuliweka mkakati na wenzangu lakini sikuwa nahisi vyema ,kwa hivyo nikaamua kutimka peke yangu “akafafanua Jeptarus
Mwanariadha huyo amesema hakuathiriwa na hali mbaya ya anga katika uwanja wa Sesi Centro Esportivo Athletics Track
“Nilikuwa nimezoea hali ya anga iliyo baridi ya hapa Brazil kwa kufanya mazoezi katika msitu baridi wa Karura nikijiandaa kwa mashindano haya jijini Nairobi”akaongeza Jeptarus .
Jeptarus amesema sasa analenga mbio za mita 800 akiwa mwingi wa matumaini kuibuka mshindi.
“Kwa sasa nasubiri ksuhiriki mbio za mita 800 ambazo nina imani nitapata ushindi I,” akasisitiza .
Jeptarus alishiriki mashindano ya dunia mwaka uliopita katika mbio za mita 1500,na mita 800 alipomaliza nafasi za nne na sita mtawalia.
Wakati uo huo Alice Atieno Odhiambo alikosa medali ,baada ya kuchukua nafasi ya nne katika urushaji sagai,matokeo yaliyomshangaza kwani hakutarajia .

Katika kuruka kwa mapana wanawake , Anzazi Chaka Nyundo alimaliza wa 6 kwenye fainali.

Kenya ni ya 11 kwenye msimamo wa nishani kwa medali 10 ,dhahabu 2 fedha 4 na shaba 4.
Dhahabu
Men’s 10000M-Simon Cherono Kibai
Men’s 1500M- Ian Wambui Kahinga
Fedha
4X400M Mix Relay
Men’s 10000M- Peter Toroitich
Women’s 10000M-Serah Wangari Kimani
Women’s 1500M- Sharon Jeptarus Bitok
Shaba
Men’s 10000M- David Kipkogei
Women’s 10000M- Grancy Kandagor
Men’s Javelin- Kelvin Kipkogei
Women’s 400M – Linet Fwamba Nanjala