Sharon Lokedi ashinda mita 10,000 majaribio ya awali ya Olimpiki Nyayo

Mwanariadha Sharon Lokedi anayeishi Marekani ameibuka mshindi wa mbio za mita 10,000 katika siku ya pili ya majaribio ya awali ya olimpiki yanayoendelea katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Lokedi ambaye pia ametimiza muda wa kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ameziparakasa mbio hizo  kwa dakika 31 sekunde 43  nukta 34  akifuatwa na Sandra Felis Chebet kwa dakika 31 sekunde 47 nukta 29  huku Nancy Jelegat akitwaa nafasi ya tatu kwa dakika  31 sekunde 49 nukta  93.

Also Read
Obiri atesa Oslo diamond league na kushinda mita 5000
Also Read
Hellen Obiri kukosa kutetea taji ya dunia ya mbio za Nyika mwaka ujao

Vane Nyabiike alichukua nafasi ya nne  kwa dakika  31 sekunde 50 nukta 50   huku Pauline Korikwang akiibuka wa tano .

Sharon Lokedi akikamilisha mita 10,000

Lokedi ambaye ana umri miaka 27 amesema amekuwa akifanya mazoezi huko Kaptagat  tangu mwezi Machi  mwaka huu baada ya kurejea kutoka  Marekani  anakosomea na sasa anajiandaa kwa majaribio ya Olimpiki yatakayoandaliwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani baina ya Juni 17 na 19.

Also Read
Wakenya waanza kwa maruerue mkondo wa kwanza wa Diamond league Gateshead Uingereza

Mashindano hayo ya siku tatu yatakamilika Jumamosi .

 

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi