Sherehe za mwaku huu za Madaraka kuandaliwa katika bustani ya Uhuru Gardens

Sherehe za mwaku huu za siku kuu ya Madaraka,zitaandaliwa katika Bustani ya Uhuru katika kaunti ya Nairobi, kwa mujibu wa katibu katika wizara ya usalama Dkt. Karanja Kibicho.

Huku akikagua maandamizi ya sherehe hizo siku ya Alhamisi, katibu huyo alisema sherehe hizo zitaandaliwa katika Bustani ya Uhuru Gardens, ili kutambua umuhiku mkubwa wa hafla hiyo.

Also Read
Wanafunzi 10 wanaofanya mtihani wa KCSE wajifungua eneo la Bomet Mashariki

Kulingana na Kibicho, maandalizi ya sherehe hizo yamekamilika asilimia 90, alidokeza kuwa Kamati andalizi ya sherehe hizo limerithika kuwapa wakenya sherehe za kufana.

Katibu huyo alisema Kamati andalizi ya sherehe za kitaifa, huenda ikakubali serikali za kaunti kuandaa sherehe sambamba na Ile ya kitaifa.

Also Read
Watu 3,000 ndio watahudhuria sherehe za Mashujaa uwanjani Gusii

Serikali ilifutilia mbali sherehe za kitaifa kuandaliwa katika viwango vya kaunti, kutokana na kuenea kwa virusi vya Covid-19.

Watu 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo, hii ikiwa ni ongezeko kutoka kwa Idadi ya awali ya watu 10,000 walioruhusiwa kutokana na Covid-19.

Also Read
Makatibu wa wizara wakagua Miradi ya Maendeleo katika eneo la Pwani

Sherehe za mwaka huu za Madaraka ndizo za mwisho chini ya utawala wa Jubilee kabla ya Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

  

Latest posts

Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Tom Mathinji

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Homa Bay wagoma wakidai kucheleweshwa kwa mishahara

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi