Shinikizo la Rais Xi kuhusu juhudi za pamoja za kupambana na covid-19 lazaa matunda

Wiki chache zilizopita zimeshuhudia ongezeko la usambazaji wa chanjo za covid-19, hasa kwa nchi zinazoendelea. Foleni ndefu za watu wanaojipanga kupewa chanjo zinaelezea hali katika vituo vingi vya afya.

Nchi za kipato cha chini, yale kutoka barani Afrika yakiongoza orodha hiyo, kwa miezi kadhaa yalikuwa yametupwa katika hali ya sintofahamu wakati chanjo vilikosa kufika, huku ukiritimba wa chanjo ukichukua usukani.

Hii ni licha ya ukweli kwamba mataifa yenye utajiri mkubwa yaliahidi msaada wa pamoja.Hali hiyo ilipokelewa kwa masikitiko makuu huku pengo la chanjo kati ya mataifa tajiri na nchi masikini likiongezeka. Shinikizo liliongezeka na mataifa yaliyoendelea yakaombwa kuacha kutoa ahadi tupu na badala yake kuchukua hatua za haraka kuokoa hali.

Haya yakiendelea, China, chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping imekuwa ikipigania umoja katika mapambano dhidi ya covid-19.

Beijing, hasa, ilitoa ahadi ya kutoa msaada ambao ungesaidia pakubwa katika mataifa masikini. China, tangu janga la Covid-19 lilipotokea, ilionyesha kuwa inachukulia kwa umuhimu mkubwa ushirikiano katika vita dhidi ya virusi hivyo.

Pamoja na upatikanaji wa chanjo, taifa hilo linaloongozwa na Chama cha Kikomunisti (CPC) lilikuwa limeahidi usambazaji sawa wa chanjo ya covid-19 kote duniani, kutokana na uwezo wake wa kuongeza kinga dhidi ya virusi hivyo hatari.

Mbali na hilo, Rais Xi amekuwa akisisitiza kuwa China itatimiza wajibu wake kama nchi yenye uwezo mkubwa, na hivyo kupigania ushirikiano katika utoaji wa chanjo ilikuwa suala la kupewa kipaumbele. Xi, kwa mfano, aliendelea kuzihakikishia nchi za Afrika kwamba taifa lake litaendelea kuunga mkono hatua za kudhibiti Covid-19 barani.

Also Read
China itaendelea kushirikiana na Afrika kupambana na malaria baada ya kuidhinishwa na WHO kuwa nchi isiyo na ugonjwa huo

Beijing ilinuia kufanya hivyo kupitia utoaji wa msaada wa kiufundi na vifaa vinavyohitajika ili kushinda virusi barani Afrika. China imekuwa ikitoa chanjo kwa nchi zinazoendelea, ambapo kufikia sasa imesafirisha chanjo kwa zaidi ya nchi 80 masikini kwa mahitaji ya haraka ya dozi hizo.Kwa sasa, nchi za Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini zinanufaika pakubwa kwa kusambaziwa mamilioni ya dozi za chanjo za Sinopharm na Sinovac.

Ni dhahiri shairi kuwa chanjo kutoka China kuelekea hadi sehemu nyingine za ulimwengu, vilichelewa kwa sababu ya kuchelewa kutolewa kwa idhini ya chanjo zake na shirika la afya duniani (WHO).Xi kila mara aliahidi kuhakikisha “utengenezaji na usambazaji wa chanjo ya COVID-19 mara utakapopatikana, utatumika kwa manufaa ya binadamu,”Kwa kutimiza ahadi hii, mwezi Mei, baada ya chanjo inayotengenezewa China aina ya Sinopharm kuorodheshwa kutumiwa kwa dharura, Beijing mara moja ilitoa michango ya dozi kwa nchi zilizoruhusu chanjo hiyo kutumika kwa raia wake.

Aidha, China iliziagiza kampuni zake za kutengeneza chanjo kuhamisha teknolojia katika nchi zinazoendelea kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa pamoja. “Hii itakuwa mchango wa China katika kuhakikisha upatikanaji wa chanjo na kwa gharama nafuu kwa nchi zinazoendelea,” alisema.Muda mfupi baadaye, chanjo kutoka China ziliongezwa kwenye mpango wa COVAX, ambao unatoa chanjo hasa kwa nchi maskini, na ambazo zinakabiliwa na matatizo ya upatikanaji wa chanjo.Hivi karibuni, chanjo kutoka China ziliongezwa kwenye kituo cha COVAX, mpango unaotoa chanjo hasa kwa nchi maskini, zinakabiliwa na matatizo ya usambazaji.”Tutaheshimu ahadi yetu ya kutoa msaada na msaada kwa nchi zinazoendelea,” alisema.

Also Read
Museveni aongoza katika matokea ya awali ya kura za Urais

Kiongozi huyo wa China aliendeleza mapambano yake dhidi ya kile alichokitaja kama utaifa wa chanjo na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutafuta suluhisho kwa masuala yanayohusu uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa chanjo, ili kuwezesha upatikanaji wa chanjo kwa urahisi katika nchi zinazoendelea.

Alifanya hivyo huku akiahidi kutoa dola bilioni 3 za Marekani kama msaada wa kimataifa kwa nchi zinazoendelea kusaidia kukabiliana na uganjwa wa COVID-19 na kusaidia kufufua uchumi katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.Itakumbukwa pia kwamba msaada wa China kwa Afrika wakati wa janga la kiafya la sasa linajumuisha misaada ya madeni kulingana na makubaliano ya mataifa ya G20 na ule wa Jukwaa la Ushirikiano wa Afrika wa China (FOCAC).

Also Read
Marekani haitakiwi kuilazimisha Afrika kuchagua kati yake na China

Na si hayo tu, msaada wa utawala wa Rais Xi kwa Afrika ulidhihirika kupitia ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa almaarufu Africa CDC jijini Addis Ababa, Ethiopia.Wakati huo huo, kiongozi huyo wa China alitangaza kuwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa Asia Mashariki itatoa dozi bilioni mbili za chanjo ya COVID-19 kwa ulimwengu kwa mwaka mzima na kutoa dola milioni 100 za Marekani kwa mpango wa COVAX.

Hii, kwa mujibu wa Xi, ni katika juhudi za kujenga jamii yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu.Kampeni yake ilikuwa na mafanikio kwani hatimaye, nchi tajiri zimeanza kuelekeza msaada wao kwa mataifa yenye uhitaji mkubwa.

Kwa sasa, usafirishaji wa chanjo barani Afrika umeongezeka, kwa karibu mara mia moja. Nchi kama vile Marekani, Uingereza, Ufaransa, Denmark, Urusi, India, na UAE zimeanza kutoa michango barani Afrika, na kutoa matumaini kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao yamewekwa hatarini na chamuko la Corona.

Ama kwa kweli, hatua za haraka za serikali ya Rais Xi kuipa Afrika vifaa vya matibabu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kupima, vifaa binafsi vya kinga (PPEs), na dawa za kusaidia mapambano, mara tu baada ya mkurupuko wa virusi vya corona ni jambo la kupongezwa.

Na Eric Biegon.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi