Shirika la KWS kuhesabu wanyamapori katika mbuga ya Amboseli

Shirika la huduma kwa wanyamapori hapa nchini KWS,litaanza zoezi la kuhesabu wanyamapori katika mbuga ya kitaifa ya Amboseli katika kaunti ya Kajiado Ijumaa wiki hii.

Naibu mkurugenzi wa KWS anayesimamia eneo hilo Lekishon Kenana, alisema shughuli hiyo itakayochukua siku nane, inanuiwa kutambua idadi kamili ya wanyamapori, maeneo halisi waliko ili kupunguza mgogoro kati ya wanyamapori na binadamu na pia kutambua hatari dhidi ya uhifadhi wa wanyamapori na usimamizi.

Zoezi hilo litaboresha juhudi za uhifadhi kwa kutambua idadi kamili ya wanyamapori pamoja na spishi zilizohatarini ili kushughulikia maswala yanayoathiri wanyamapori,” alisema Kenana.

Kenana aliyezungumza katika kaunti ya Kajiado alisema kinyume na hapo awali ambapo waliangazia sana kuwahesabu Ndovu,Simba,Kifaru,Nyati na Chui, wakati huu wanyamapori wote watahesabiwa.

Kulingana na mkurugenzi huyo, habari zitakazokusanywa, zitatumika kuboresha utekelezwaji wa sera za uhifadhi na zile za utalii hapa nchini.

Tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu, Kenya ilizindua zoezi la kwanza la kuhesabu wanyamapori ili kutambua hali ya raslimali ya wanyamapori ilivyo hapa nchini.

Shughuli hiyo ya miezi miwili inayofadhiliwa na serikali kwa kitita cha shilingi milioni 250,itatekelezwa na wizara ya utalii na uhifadhi wanyamapori, Shirika la kitaifa la kuhifadhi wanyamapori nchini na taasisi ya mafunzo ya utafiti wa wanyamapori nchini.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi