Shirika la NMS lafanyia majaribio kituo cha magari cha Green Park

Huduma ya jiji la Nairobi (NMS) Jumanne asubuhi, iliandaa zoezi la majaribio ya kituo cha kuegesha magari ya uchukuzi wa umma cha Green Park Jijini Nairobi.

Magari yote ya uchukuzi wa umma yanayohudumu katika mitaa ya Ngong, Kibra, Rongai, na Dagoretti yalishukisha abiria katika kituo hicho kipya cha Green Park.

Also Read
Watu 57 wahukumiwa kuhudumia jamii kwa kukiuka masharti ya kudhibiti Covid-19

Mkurugenzi wa barabara wa huduma ya NMS mhandisi Michale Ochieng aliyeongoza zoezi hilo, alisema ujenzi wa kituo hicho utakamilika hivi karibuni kabla ya uzinduzi rasmi mwezi ujao.

Ochieng alisema zoezi hilo la majaribio litawapa nafasi ya kutambua mianya iliyopo kwa nia ya kuhakikisha kila kitu kishwari kabla ya uzinduzi.

Also Read
Ngatia: Uhusiano wangu na Rais Kenyatta hautahujumu uhuru wa Mahakama

Ujenzi wa kituo hicho ni mojawapo wa mipango ya huduma ya jiji la Nairobi NMS, kupunguza msongamano wa magari jijini kwa kuyaondoa kwa awamu magari ya uchukuzi wa abiria kutoka sehemu ya katikati mwa jiji.

Also Read
Watu 14 zaidi wafariki huku wengine 968 wakiambukizwa virusi

Abiria walioabiri magari yaliyotamatisha safari zake katika kituo hicho walikuwa na maoni mesto, waliounga mkono hatua hiyo wakisema itarahisisha usafiri kuingia na kutoka jijini.

Magari yote ya uchukuzi wa umma yanayotumia barabara za Ngong na Langanta yatakuwa yakibeba na kuwashukisha abiria katika kituo hicho.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi