Shughuli za Kampeini zasitishwa katika maeneo bunge ya Bonchari na Juja

Shughuli zote za kampeini kwa chaguzi ndogo za maeneo-bunge ya Juja na Bonchari zilisitishwa Jumamosi jioni huku wawaniaji wote wakifanya juhudi za mwisho mwisho kuwashawishi wapigaji kura.

Katika eneo-bunge la Bonchari, muwaniaji wa chama cha ODM, aliye pia mkurugenzi mkuu wa zamani wa halmashauri ya udhibiti wa kawi humu nchini, Mhandisi Pavel Oimeke alikuwa katika eneo la Suneka huku kampeini zikiingia awamu za mwisho.

Also Read
Mwakilishi wadi ya Kiamokama katika bunge la kaunti ya Kisii Kennedy Mainya ameaga dunia

Gavana wa kaunti ya Kisii, James Ongwae alikuwa kwenye kanisa la Bigogo SDA, lililoko wadi ya Bomariba, eneo-bunge la Bonchari kwa maombi ya Sabato ambapo alihimiza wakaazi kumchagua kuwaniaji wa chama cha ODM.

Seneta wa Kisii Prof. Sam Ongeri, na katibu mkuu wa ODM- Edwin Sifuna, walikuwa kwenye kanisa la Kerina Central SDA, huko Bonchari ambako walihimiza wakaazi kumchagua Oimeke kutokana na ujuzi wake katika maswala ya uongozi.

Also Read
Chama cha kitaifa cha matabibu chatishia kuandaa mgomo wa kitaifa

Uchaguzi mdogo wa eneo-bunge la Bonchari, umevutia wawaniaji 13, wote wakitaka kuchaguliwa mahala pa mbunge John Oroo Oyioka ambaye alifariki miezi mitatu iliyopita.

Katika eneo-bunge la Juja, mambo yalikuwa ni vivyo-hivyo huku wawaniaji wote wakitamatisha kampeini zao.

Also Read
Wafanyibiashara wa Soko la Mung’etho huko Kiambu walalamikia unyakuzi wa ardhi ya soko lao

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha mbunge wa Juja Francis Waititu, kwa jina maarufu “Wakapee” mnamo tarehe 23 Februari.

Kiti hicho kimeshuhudia kinyang’anyiro kikali baina ya mjane wa mbunge huyo Susan Njeri Waititu wa chama cha Jubilee na George Koimburi wa “People’s Empowerment party.

  

Latest posts

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi