Shughuli za kibiashara zimeanza katika mradi wa Galana/Kulalu

Serikali ya Kenya imeanzisha shughuli za kibiashara kwenye mradi wa shamba la ekari elfu kumi la Galana/ Kulalu ulio katioka kaunty za kilifi na Tana River, hayo ni kwa mujibu wa waziri wa maji na unyunyizaji maji mashamba Sicily Kariuki.

Kwa mujibu wa Kariuki, wizara yake  kwa ushirikiano na wizara ya fedha, zinamtafuta mwekezaji wa humu nchini au wa kimataifa kuendelea na kazi kwenye mradi huo punde tu wakati halmashauri ya kitaifa ya unyunyizaji maji mashambani itakapokamilisha miundo msingi kwenye shamba  hilo.

Also Read
IEBC kusajili zaidi ya wapiga kura 4,000 wapya Kilifi
Waziri wa maji na unyunyizaji maji mashamba Sicily Kariuki katika mradi wa Galana/Kulalu.

Alikariri kwamba wizara yake kupitia halmashauri ya unyunyizaji maji mashambani inakaribia kukamilisha miundo msingi katika shamba la ekari 4,900 lililosalia kabla ya kukabidhi mradi huo kwa sekta ya kibinafsi.

Also Read
Kenya kukabwa koo na makali ya kiangazi huku mvua chache ikitarajiwa

Waziri huyo ambaye alikagua mradi huo, alisema awamu ya pili ya mradi huo imekamilika kwa asilimia 72 na inapaswa kuwa tayari kwa shughuli za kibiashara kufikia mwezi Januari mwaka 2022.

Also Read
Aaron Cheruyiot kuchunguzwa na NCIC dhidi ya matamshi ya uchochezi

Kariuki alidokeza kuwa mradi huo wa Galana/Kulalu ulioanza miaka saba iliyopita, ni mkakati wa serikali unaonuia kuongeza mashamba yaliyo chini ya unyunyizaji maji kutoka ekari 540,000 hadi zaidi ya ekari milioni moja hapa nchini chini ya ule mpango wa ruwaza ya mwaka 2030.

  

Latest posts

Kennedy Obuya asimulia jinsi mchezo wa Ckricket ulivyobadilisha maisha yake

Dismas Otuke

Watu 19 wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni Kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Watu wawili zaidi wametolewa katika migodi ya Abimbo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi