Shujaa kuanza kampeini ya Olimpiki dhidi ya Marekani

Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upande maarufu kama Shujaa itaanza harakati za kuwania taji ya Olimpiki katika kundi C dhidi ya Marekani Julai 26 katika uwanja wa Tokyo.

Shujaa chini ya ukufunzi wa Innocent Simiyu  itarejea uwanjani  siku hiyo dhidi ya Afrika Kusini kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya Ireland tarehe 27 mwezi huu.

Also Read
Shujaa kuanza mazoezi ya Olimpiki Novemba

Shujaa itasafiri baina ya Julai 9 na 10 kwenda Japan ambapo itakita kambi ya mazoezi mjini Kurume  Japan kabla ya kuelekea Tokyo tarehe 19 mwezi huu.

Also Read
Keter na Chepkirui washinda mita 1500 na kufuzu kwa mashindano ya dunia Kasarani

Kenya inashiriki Olimpiki kwa mara ya pili baada ya kushiriki mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro Brazil.

Katika mechi ya ufunguzi ya raga mabingwa watetezi  Fiji wataanza kibarua dhidi ya  wenyeji Japan katika kundi  B Julai 26 .

Also Read
Misri na Ivory Coast zatinga kwota fainali ya Olimpiki

Fainali ya kuwania medalia itapigwa tarehe  28 mwezi huu.

Timu ya akina dada ya Kenya maarufu  kama Lionesses itashuka uwanjani kwa pambano la kwanza la kundi  A, dhidi ya Newzealand  kabla ya kugaragazana na Uingereza tarehe 30.

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi