Shujaa kupambana na Ujerumani robo fainali ya kombe kuu msururu wa Edmonton Jumapili usiku

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upande, Shujaa itashuka uwanjani kupambana na Ujerumani katika robo fainali ya kombe kuu katika mkondo wa pili wa Hsbc wa Edmonton nchini Canada Jumapili saa moja na dakika 4 usiku.

Also Read
Shujaa kupiga kambi ya Mazoezi mjini Stellenbosch kwa siku 10

Shujaa imemaliza ya pili katika kundi B kwa pointi 7 baada ya kushinda mechi mbili na kupoteza mmoja.

Kenya iliwazidia maarifa Chile pointi 38-5 katika pambano la kwanza Jumamosi kabla ya kuwaangusha Uhispania alama 26-12 lakini wakapoteza kwa USA alama 14-19 katika mechi ya mwisho mapema Jumapili.

Also Read
Shujaa wabanduliwa Olimpiki baada ya kuporomoshwa na Ireland 7-12

Ni mara ya pili mtawalia kwa shujaa kutinga kwota fainali ya kombe kuu baada ya kuibuka ya pili katika msururu wa kwanza wiki iliyopita huko Vancouver Canada na kujizolea pointi 18.

Also Read
Shujaa yazidiwa maarifa na Argentina kwa mara tatu Madrid 7's

kwenye ratiba nyingine ya robo fainali kuwania kombe kuu USA watakabana koo na Uingereza,Ireland iwe na miadi na wenyeji Canada huku Afrika Kusini wakimenyana na Hong Kong 7’s.

  

Latest posts

Dismas Otuke

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Rais wa zamani wa shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF Lamine Diack afariki akiwa na umri wa miaka 88

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi