Shujaa wabanduliwa Olimpiki baada ya kuporomoshwa na Ireland 7-12

Shujaa imebanduliwa nje ya michezo ya Olimpiki mapema Jumanne ,baada ya kuambulia kichapo cha alama 7-12 dhidi ya Ireland katika pambano la mwisho la kundi C katika uwanja wa Tokyo .

Kenya ilikuwa chini alama 12-0 kabla ya Vincent Onyala kufunga try na Conversion .

Also Read
NOCK yazindua maafisa watano wa kiufundi kuingoza Kenya kwa michezo ya Olimpiki

Kenya awali ilikuwa imecharazwa na  USA alama 14-19 na  5-14 dhidi ya Afrika Kusini katika mechi za ufunguzi Jumatatu na hivyo basi kuyaaga mashindano ya Olimpiki bila kushinda mechi matokeo ambayo ni sawa na yale ya mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro ilipopoteza michuano yote mitatu.

Also Read
Vitanda vya Olimpiki vimeundwa kwa Card board

Shujaa watarejea uwanjani Tokyo saa tano asubuhi ya Jumanne dhidi ya wenyeji Japan katika mkwangurano wa kuwania  nafasi za 9 hadi 12.

Also Read
Kocha na mchezaji wa zamani wa Shujaa Benjamin Ayimba afariki akiwa na umri wa miaka 44

Katika mechi za kwota fainali Newzealand wameratibiwa kuchuana na  Canada,Uingereza dhidi ya USA, Australia dhidi ya mabingwa watetezi Fiji wakati Afrika Kusini ikiwa na miadi dhidi ya Argentina.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi