Shujaa yaibuka ya tatu mkondo wa kwanza wa Dubai 7’s

Timu ya raga ya Kenya kwa wanaume 7 upande ilimaliza ya tatu katika mkondo wa kwanza wa mashindano ya Dubai 7’s yaliyokamilika Jumamosi.

Shujaa iliwacharaza Japan  pointi 31-14 katika mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne ,baada ya kushindwa kwenye nusu fainali ya kombe kuu alama 5-17 na Ufaransa.

Also Read
Shujaa na Lioness kujipima makali Madrid 7's

Awali Kenya ilikuwa imeipakata Canada pointi 21-19 katika robo fainali ya kombe kuu,na kabla ya hapo katika mechi za makundi walipoteza alama 14-15 dhidi ya Uhispania kabla ya kutoka sare ya 19-19 na Ufaransa na kuisasambua Chile pointi 39-7 na kumaliza ya tatu kundini.

Also Read
Chama cha soka Uingereza chalaani ubaguzi wa rangi

Argentina walitwaa kombe kuu kufuatia ushindi wa alama 19-7 dhidi ya Ufaransa ,wakati Uganda ikichukua nafasi  ya 7 kwa kuinyuka Uhispania alama  24-19.

Also Read
Simba yaitafuna Vita hadharani

Mkondo wa  pili wa mashindano hayo utaandaliwa wikendi ijayo huku timu ya Kenya ikiyatumia kujinoa kwa michezo ya Olimpiki Mjini Tokyo Japan.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi