Shujaa yamaliza ya pili mkondo wa kwanza wa Solidarity Camp mjini Stellenbosch

Timu ya Kenya ya raga kwa wanaume 7 upande almaarufu Shujaa iliibuka ya pili huku mkondo wa kwanza wa mashindano ya Solidarity Camp ukikamilika Jumapili usiku mjini Stellenbosch Afrika Kusini.

Also Read
Kikosi cha Kenya Lioness kwa mashindano ya Madrid 7's chatajwa

Shujaa chini ya ukufunzi wa Innocent Simiyu ilipoteza mchuano wa fainali dhidi ya Blitzboks ya Afrika Kusini pointi  7-31.

Ilikuwa mechi ya pili kwa Kenya kupoteza dhidi ya Afrika Kusini ,baada ya kushindwa alama 17-27 siku ya Jumamosi .

Also Read
Mancity waafikiana kumsajili beki Ruben Dias kutoka Benfica

Mtaifa yanayoshiriki mashindano hayo ni Uganda,Zimbabwe,Afrika Kusini na Kenya huku mataifa  ya Kenya na Afrika Kusini yakitumia michuano hiyo kujipiga msasa kwa michezo ya Olimpiki makala ya 32 kati ya  Julai 23 na Agosti 8 mwaka huu.

Also Read
Shirikisho la riadha ulimwenguni laridhishwa na maandalizi ya Kenya ya mashindano ya Chipukizi

Mkondo wa pili na wa mwisho wa Solidarity camp  utaandaliwa kati ya Mei 14 na 15 .

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi