Shujaa yashindwa fainali ya kombe kuu na Afrika Kusini 5-38 Vancouver 7’s

Timu ya taifa ya Kenya ya raga kwa wachezaji 7 upande maarufu Shujaa ilipoteza alama 5-38 na Afrika Kusini mapema Jumatatu katika fainali ya kombe kuu kwenye msuru wa kwanza wa dunia wa IRB huko Vancouver Canada .

Angelo Davids aliifungia Afrika Kusini maarufu kama Springboks tries za kwanza mbili dakika ya 2 na 5 kabla ya Sokoyisa Makata na Ronald Brown kungeza try moja kila mmoja na kuongoza alama 24-0 kufikia mapumziko.

Also Read
Shujaa kuanza mazoezi ya Olimpiki Novemba

Kipindi cha pili Christie Grobebbelaar na Darr Adonis Adoni walipachika try moja kila mmoja huku ile ya pekee ya Kenya ikifungwa na Daniel Taabu.

Also Read
Shujaa yaripoti kambini kwa mashindano ya kirafiki Afrika Kusini

Shujaa ambayo iliwajumuisha wachezaji wengi chipukizi ilifungua msururu huo kwa ushindi wa alama 17-5 dhidi ya Uhispania siku ya Jumamosi , kabla ya kuiparamia Mexico kwa kuinyuka pointi 45-7 na kushindwa na Afrika Kusini katika mchuano wa mwisho mapema Jumapili alama 14-33.

Katika hatua ya Robo fainali ya kombe kuu Kenya iliwacharza USA alama 19-14 na hatimaye kuwalaza Ireland 38-5 kwenye nusu fainali.

Also Read
Ongare atinga raundi ya pili baada ya kumzaba Mrundi Ornellein mashindano ya Zone 3

Shujaa ni pili kwenye msimamo kwa alama 18 na watasalia nchini Canada kushiriki msururu wa pili wa Edmonton baina ya tarehe 25 na 26 mwezi huu.

  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi