Shujaa yatota baada ya kuambuliwa 14-19 na USA Olimpiki

Timu ya taifa ya raga ya Kenya ya raga kwa wachezaji 7 kila upande ya wanaume maarufu kama Shujaa imeanza vibaya kampeini ya Olimpiki ,baada ya kushindwa  alama 14-19 na Marekani katika mechi ya kundi C iliyopigwa mapema Jumatatu katika uwanja wa Olimpic mjini Tokyo Japan.

Also Read
Azzuri waiduwaza Uingereza nyumbani na kunyakua kombe la Euro

USA ilikuwa ikiongoza pointi 10-0 kufikia mapumzikoni kabla ya nahodha wa mechi hiyo Collins Injera kufunga try 1 na conversion  naye Jeff Oluoch akaongeza  try nyingine moja huku Eden Agero akiipatia Kenya alama 4.

Also Read
Shujaa kuanza mazoezi ya Olimpiki Novemba

Shujaa watarejea uwanjani saa saba adhuhuri kwa mechi ya pili dhidi ya Afrika Kusini kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya Ireland mapema Jumanne.

Also Read
Huenda vipindi vya michezo ya kamari vikapigwa marufuku katika vyombo vya habari

Shujaa inasaka ushindi wa kwanza katika michezo ya Olimpiki baada ya kupoteza mechi zote tatu katika malaka ya mwaka 2016 mjini Rio  Brazil.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi