Shujaa yazidiwa maarifa na Argentina kwa mara tatu Madrid 7’s

Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upnde imepoteza kwa Argentina pointi 19-36 katika mechi ya mwisho Jumapili alasiri katika mashindano ya Madrid 7’s.

Shujaa chini ya ukufunzi wa Innocent Simiyu ilikuwa nyuma alama 7-24 kufikia mapumzikoni Try ya pekee yaKenya ikifungwa na Bush Mwale kabla ya kujipatia alama nyingine mbili kwa Conversion.

Also Read
Azzuri waing'atua Ubelgiji na kufuzu kwa semi fainali ya Euro

Argentina walitanua uongozi wao hadi alama 7-31,kabla ya Jacob Ojee kupiga try ya pili wakati Daniel Taabu akifunga conversion na kupunguza pointi hadi 14-31, na kisha baadae Ojee akapiga try ya pili huku Taabu akikosa conversion na hadi kipienga cha mwisho Kenya wakapoteza alama 19-36.

Also Read
Lionesses waanza vibaya mashindano ya Dubai 7's

Awali Shujaa waliikomoa Chile 15-5 katika mechi ya kwanza na ushinde dhidi ya Argentina ulikuwa wa tatu mtawalia baada pia ya kulemewa na timu hiyo ya Amerika kusini wiki jana.

Also Read
Vikosi vya Shujaa na Lionesses kwa mashindano ya Emirates Dubai 7's vyatajwa

Matokeo ya Jumamosi Februari 27

FT: Kenya 26-12 Portugal,
FT: Kenya 29-12 USA,
FT: Kenya 19-17 Spain,

  

Latest posts

Emmanuel Korir avunja nuksi na kushinda dhahabu ya kwanza ya Kenya Olimpiki mita 800

Dismas Otuke

Chemutai wa Uganda awaduwaza Wakenya na kunyakua dhahabu ya kwanza ya Olimpiki mita 3000 kuruka viunzi na maji

Dismas Otuke

Sydney McLaughlin avunja rekodi ya dunia ya mita 400 kuruka viunzi wanawake katika Olimpiki

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi