Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Ni afueni kwa shule za umma na zile za kibinafsi baada  wizara ya habari, teknolojia na mswala ya vijana kuzindua mpango wa kuunganisha shule na mitandao ya Internet.

Kulingana na wizara hiyo, takriban shule 43,000 zitaunganishwa na mtandao wa internet kote nchini huku shule 1,000 tayari zikiwa zimetambuliwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo.

Also Read
Visa 735 vipya vya Covid -19 vyanakiliwa huku watu 12 zaidi wakifariki hapa nchini

Katibu mwandamizi katika wizara ya habari, teknolojia na mswala ya vijana Maureen Mbaka alisema mradi huo unaofadhiliwa na shirika la umoja wa mataifa ya hazina ya watoto UNICEF, utatekelezwa kwa awamu nne.

Also Read
Watu kadhaa wajeruhiwa kwenye ajali nyengine ya Barabara Kuu ya Malindi kuelekea Mombasa

Kulingana na Katibu huyo mwandamizi,  tokana na mradi huo shule zitapokea mtandao wa internet wa kasi ya 10MBPS ili ziweze kupata vifaa vya masomo mtandaoni bila tatizo.

Mbaka alitangaza kuwa wizara ya ICT imebuni tovuti ya masomo ya mtandaoni ili kuwawezesha walimu katika maeneo ya mashinani kutumia mpango wa masomo ya Dijitali wakiwa nyumbani.

Also Read
Gachagua ashtakiwa kwa makosa ya ufisadi katika Mahakama ya Milimani

“Tumeshirikiana na asasi nyingine kama vile Halmashauri ya mawasiliano nchini, wizara ya elimu na washirika wa sekta ya kibinafsi  kubuni mbinu za kuhakikisha wanafunzi wnapata teknolojia ya masomo wakiwa nyumbani,” alisema Mbaka.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi