Shule tano zafungwa Laikipia Magharibi kutokana na utovu wa usalama

Hatima ya wanafunzi 2, 000 katika eneo-bunge la Laikipia Magharibi ambalo linakumbwa na kero la utovu wa usalama  haijulikani, baada shule zao kufungwa kutokana na uvamizi unaotekelezwa na majambazi na wizi wa mifugo katika eneo hilo.

Shule hizo tano za msingi ni pamoja na Wangwachi, Bondeni, Kabati, Mirango na  ile ya sekondari ya kutwa ya Kabati zilisalia kufungwa hata baada ya nyingine kote nchini kurejelea masomo kwa muhula wa kwanza.

Also Read
Ruto: Orodha ya mali yangu iliyowasilishwa bungeni ni ya kupotosha

Wazazi kutoka maeneo hayo yaliyoathirika wanaendelea kuhofia usalama wa wanao.

Siku ya Jumatano na Alhamisi, zaidi ya maboma 20 katika vijiji vya Wangwachi na Bondeni, wadi ya Ol Moran ambayo inapakana na eneo hatari la hifadhi Laikipia,walivamiwa huku idadi ya mifugo isiyojulikana ikiibwa na wavamizi waliojihami kwa silaha.

Also Read
Hatma ya Mike Sonko sasa imo mikononi mwa bunge la Senate

Wakazi hao wanasema mamia ya mifugo wameibwa licha ya operesheni ya kunyang’anya watu silaha ikiendelea kutekelezwa.

Also Read
Wakenya kuanza kupokea Huduma Namba Desemba

Aidha wakazi hao wanatoa wito kwa waziri wa usalama kitaifa Dkt Fred Matiang’i kuigilia kati wakisema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kudumisha amani katika maeneo ya wafugaji huko Laikipia Kaskazini huku mafugaji wadogo-wadogo wakibaguliwa katika eneo la Laikipia Magharibi.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi