Shule ya wasichana ya Lugulu yafungwa kufuatia ghasia za wanafunzi wanaolalamikia ubakaji

Shule ya upili ya wasichana ya Lugulu kwenye Kaunti ya Bungoma imefungwa baada ya ghasia za wanafunzi kufuatia madai ya kubakwa kwa mmoja wao.

Wanafunzi hao waliandamana Jumanne kulalamikia kisa cha kubakwa kwa mmoja wao alipokuwa akioga kwenye bafu siku ya Jumamosi kabla ya masomo ya asubuhi.

Also Read
Baraza awarai wakaazi wa Bungoma kujiandikisha kwa wingi kupiga kura

wanafunzi hao wapatao 306 walitembea mwendo wa kilomita sita kutoka shuleni kwao hadi Kituo cha Polisi cha Webuye wakiwa wamebeba mabango yaliyoshinikiza kukamatwa mara moja kwa mshukiwa wa kitendo hicho.

Also Read
Mauaji ya mwanaume yasababisha mshikemshike mtaani Kayole

Walimshtumu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Dinnah Cheruiyot kwa kukosa kuchukua hatua ya haraka dhidi ya aliyetekeleza kitendo hicho ambaye wanataka atiwe mbaroni.

Bodi ya usimamizi wa shule hiyo imeagiza kufungwa kwa taasisi hiyo huku polisi wakichunguza kisa hicho.

Also Read
Gavana Susan Kihika afutilia mbali deni la bili za hospitali la shilingi bilioni tano

Afisa Mkuu wa Polisi kwenye Kaunti Ndogo ya Bungoma Mashariki Valerian Obore amewataka wanafunzi walio na ushahidi kuhusu  tukio hilo kuandikisha taarifa ili kusaidia katika uchunguzi.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi