Shule za Garissa ziko tayari kwa ufunguzi, wasema Wakuu wa Elimu

Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Garissa Khalif Isaack Hassan amedokeza kuwa shule zote za umma katika kaunti hiyo ziko tayari kufunguliwa Jumatatu kulingana na tangazo la Wizara ya Elimu.

Khalif amesema walimu, wasimamizi na wafanyikazi wengine wa shule tayari wamepokea mafunzo kuhusu kanuni za Wizara ya Afya na wako tayari kupokea wanafunzi hao.

“Tumewahamasisha walimu wetu kuhusu kanuni za Wizara ya Afya. Pia tumewahusisha wasimamizi wa shule na wafanyikazi wengine katika mchakato huo kwa sababu ni sehemu ya jamii ya shule hizo,” ameeleza Khalif.

Also Read
Serikali ya kaunti ya Garissa yasambaza chakula kwa familia zisizojiweza

Khalif ameongeza kuwa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa katika vyuo vya eneo hilo walirejelea masomo Jumatatu.

Naye Katibu wa Chama cha Walimu nchini KNUT, tawi la Garissa, Abdirizak Hussein ameisifu Wizara ya Elimu kwa kuchukua hatua hiyo ya ufunguzi wa shule.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Shule ya Msingi ya Garissa, Abdirizak amesema janga la COVID-19 litadumu kwa miezi au miaka kwa hivyo shule haziwezi kuendelea kufungwa.

Also Read
John Mutua Katuku aidhinishwa na IEBC kuwania Useneta wa Machakos

“Tunaamini kuwa Wizara ya Elimu itakuwa imezingatia kanuni zote za Wizara ya Afya wakati shule zitakapoanza kufunguliwa Jumatatu kama ilivyotangazwa na Waziri Magoha,” akasema.

Hata hivyo, baadhi ya wazazi wamepinga hatua hiyo ya ufunguzi wa shule wakiitaja kama mpango uliokimbiliwa unaoweza kuleta madhara mabaya.

Kulingana na David Musyoka ambaye ni mzazi katika eneo hilo, nchi hii huenda ikapoteza ufanisi wote ulioafikiwa katika juhudi za kukabiliana na msambao wa COVID-19.

“Kwa nini tukimbilie kufungua shule wakati tunajua virusi vya Corona bado ni tishio kwa afya ya Wakenya? Mwezi Agosti, Waziri Magoha alitangaza kuwa mwaka wa masomo wa 2020 umefutiliwa mbali kwa sababu ya janga la COVID-19. Miezi miwili baadaye, anakimbilia kufungua shule. Ni kitu gani kimebadilika?” Akauliza Musyoka.

Also Read
Abdulkadir Haji ameapishwa kuwa Seneta mpya wa kaunti ya Garissa.

Zainab Abdi naye analalamika kuwa wazazi wengi hawako tayari kwa ufunguzi wa shule Jumatatu.

“Serikali inajua kabisa kuwa Wakenya wengi walipoteza ajira zao kufuatia janga la COVID-19. Mbona inakimbilia kufungua shule?” Akashangaa.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi