Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Mkurugenzi wa elimu katika eneo la  Lugari Magdalene Igwatai amesema shule za umma zina walimu waliohitimu vyema zaidi na vitabu vya kutosha vya ki-ada hali ambayo inaziweka katika nafasi bora kuwa-anda wanafunzi kufanya vyema katika mitihani.

Igwatai alikuwa akiongea wakati wa kutolewa kwa matokeo ya kwanza ya mtihani wa majaribio wa muhula wa kwanza kwa madarasa ya saba na nane kwa zaidi ya shule 75 za msingi za umma na za kibinafsi katika shule ya Kingdomsons Academy.

Also Read
Jamii ya Ogiek yataka irejeshwe katika msitu wa Mau

Alitoa changamoto kwa walimu wa shule za umma kutotegemea sababu zisizokuwa za kimsingi kwa matokeo duni ya mitihani na badala yake kujitahidi kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaandikisha matokeo bora.

Also Read
Kenya yanakili visa 572 vipya vya Covid-19

Deborah Ongidi, ambaye ni mkurugenzi wa tume ya kuwaajiri walimu nchini wa kaunti ndogo ya Lugari, aliyehudhuria hafla hiyo alielezea umuhimu wa walimu wakuu katika kuhakikisha shule zinaandikisha matokeo bora.

Also Read
Rais Kenyatta: Serikali imejitolea kulinda mipaka ya nchi hii

Ongidi hata hivyo alisema utoaji ushauri nasaha na kuwapa wanafunzi ujuzi katika viwango vya elimu ya msingi, unapaswa kuchukuliwa kwa makini na walimu wakuu kwani wanafunzi huwa wanaandaliwa vyema katika maisha yao ya baadaye.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi