Sifuna: ODM haina lengo la kuvuruga shughuli za uteuzi

Chama cha Orange Democratic Movement, hakina nia ya kuvuruga shughuli za uteuzi wa chama hizo zinazoendelea kote nchini, haya yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna.

Sifuna aliyezungumza siku ya Jumanne asubuhi katika mahojiano na kituo cha Radio Taifa cha shirika la utangazaji nchini KBC, alitoa wito kwa wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu, chama hicho kinapoandaa uteuzi katika kaunti ya Kisumu siku ya Jumanne.

Also Read
Raila hategemei kuidhinishwa na Uhuru ili kugombea urais, wasema baadhi ya viongozi wa ODM

“Chama cha ODM hakiwezi vuruga shughuli ya uteuzi kwa njia yoyote. Wanashukuru wafuasi wote wa ODM kwa kushiriki uteuzi kwa njia ya amani. Tunawasihi wale wote wanaoshiriki zoezi hilo kudumisha amani tunapokamilisha zoezi hilo,” alisema Sifuna.

Also Read
Bahati Aandaa Mkutano wa Maombi na Baadhi ya Wakazi wa Mathare

Chama hicho kinatarajiwa kuandaa shughuli ya uteuzi katika kaunti ya Kajiado na Narok siku ya Jumatano na katika kaunti ya Nairobi siku ya Alhamisi.

Alidokeza kuwa ODM ni chama cha pekee ambacho kimekumbatia utumizi wa teknolojia katika shughuli zake za uteuzi, na kuwahakikishia wanachama kuwa shughuli hiyo itakuwa huru na ya haki.

Also Read
Kura ya maoni yamweka Naibu Rais William Ruto kifua mbele dhidi ya wawaniaji urais

“Teknolojia tuliyo nayo, haiwezi vurugwa. Tutafungua Sava kwa wawaniaji ambao watashuku mchakato huo,” alisema Sifuna.

Alitoa wito kwa vyama tanzu ndani ya muungano wa Azimio La Umoja One Kenya kujiepusha na kushinikiza masilahi ya kibinafsi.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi