“Sijapata mtoto” asema Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee amelazimika kutangaza kwamba hajapata mtoto.

Hii ni baada ya mmoja wa wafuasi wake kwenye Instagram kuandika maneno “It’s a boy” chini ya picha ambayo Vanessa alikuwa amechapisha na maneno “But God”.

Kwenye video ya kukana madai ya kujaliwa mtoto wa kiume Vanessa anasikika akikanya wafuasi wake waache kusambazwa habari hizo maanake wanazua wasiwasi Kati ya watu wake wa karibu kama vile mamake mzazi.

Also Read
Yul Edochie atofautiana na babake

Vanessa alichumbiwa na mpenzi wake mwanamuziki wa Marekani mwenye asili ya Nigeria Rotimi ambaye pia ni muigizaji, mwisho wa mwaka 2020 baada yao kuishi pamoja kwa muda.

Also Read
Harambee Stars kupimana nguvu tena na Taifa Stars Alhamisi saa tisa Nyayo Stadium

Wawili hao hawajasema ikiwa watafanya harusi.

Mwezi Mei mwaka huu wa 2021, Vanessa alichapisha picha ambazo zinaonyesha yeye na Rotimi wakiwa wanajivinjari katika visiwa vya Antigua na Barbuda na watu wakakisia kwamba ana ujauzito.

Japo hajawahi kusema lolote kuhusu jambo hilo.

Wanawake mitandaoni wamekuwa wakitamani maisha ya mwanadada huyo mzaliwa wa Tanzania ambaye alipata elimu ya chuo kikuu nchini Kenya baada yake kuchapisha video ambayo inaonyesha mchumba wake Rotimi akimhesabia dola nyingi huku akimwelezea jinsi ya kuzitumia.

Also Read
Samia Suluhu kuapishwa kama rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania

Vanessa aliamua kuacha muziki ili kuwa na muda na mchumba wake Rotimi huko Marekani isijulikane kama baadaye atarejea kwenye fani hiyo.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi