Simba SC Yampumzisha Mchezaji Bernard Morrison

Mchezaji soka Benard Morrison amepatiwa likizo na usimamizi wa timu ya Simba Sc ambayo amekuwa akiichezea nchini Tanzania hadi mwisho wa msimu huu. Taarifa ya afisa mkuu mtendaji wa Simba SC Bi. Barbara Gonzalez haikufafanua kikamilifu sababu za hatua hiyo lakini inasema kwamba wanampa muda ashughulikie matatizo yake ya kibinafsi na wanamtakia kila la heri katika mapumziko na safari yake ya soka baadaye.

Gonzalez kwenye taarifa yake alitambua mchango muhimu wa mchezaji huyo kwa timu ya Simba kwa miaka miwili ambayo amekuwa akiichezea kama vile kwenye robo ainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika mara mbili. Ushindi wa Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi umetajwa pia kwenye mafanikio ya Simba aliyochangia Morrison.

Also Read
Shilole na Rommy wafunga ndoa

Bernard Morrison pia alitangaza likizo hiyo ambapo alisema inatokana na matatizo ya kifamilia ambayo yanamzidi na ambayo yangeathiri ubora wake kama mchezaji. “Kuna mengi yanastahili kusemwa kuhusu mapumziko haya lakini kwa sasa ninatakia timu mema kwa michuano iliyosalia. Natumai nitayatatua haraka ili niweze kujiunga tena na timu.” ndiyo baadhi ya maneno ya Morrison.

Also Read
Rais mcheshi azindua kitabu

Lakini wapo wakereketwa wa soka Tanzania ambao wanahisi kwamba wakati ulikuwa umewadia wa Simba Sc kumwachilia Bernard Morrison. Juma Ayo aliandika, “Hongereni sana uongozi wa Simba kwa kuachana na Morison hata msingezungukazunguka na likizo ya milele, mngesema mmeachana naye. Alikuwa anaharibu jina na nembo ya klabu! Nidhamu hakuwa nayo na timu ilikuwa inakosa huduma zake kwenye matukio ya muhimu kwa sababu ya nidhamu.”

Also Read
Suluhu alionya Bunge la Tanzania dhidi ya kumfananisha na Pombe

Kati ya matukio mabaya ya Morrison ni moja la mwaka 2020 ambapo mchezaji huyo wa asili ya Ghana alipigwa marufuku ya mechi tatu kwenye mechi ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kuzozana na mchezaji Juma Nyoso ambaye pia aliadhibiwa.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Mataifa ya G7 kusitisha uagizaji dhahabu kutoka Urusi

Tom Mathinji

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi