“Sitaki mchezo kwa watoto wangu!” asema Shilole

Mwanamuziki wa Tanzania aliyepia mjasiriamali Zuena Yusuf Mohamed maarufu kama Shilole au Shishi amezungumzia jinsi analinda na kutunza mabinti zake kuhu akiwaweka mbali na watu ambao huenda wakawadhuru.

Mwanadada huyoalikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi Fm aliyetaka kujua ni kwa nini Shishi ameficha watoto wake kutoka kwenye mitandao ya kijamii tofauti na watu wengine maarufu ambao wanaweka watoto wao hadharani na hata wakati mwingine kuwafungulia akaunti za mitandao ya kijamii hata wakiwa wachanga.

Also Read
Akaunti ya Nameless ya Instagram yadukuliwa

Shilole alisema yeye alichagua kuishi maisha ya kuwa kwenye jicho la umma lakini hataki kuchagulia watoto wake maisha hayo kwa sasa, alisema kitu ambacho amewachagulia kwa sasa ni elimu bora ili wawe wanawake wa maana siku za usoni.

Alifichua kwamba binti zake hata simu hawana na hawaruhusiwi kuwa nayo na kwamba wanapokuwa nyumbani wanasoma elimu ya dini ya kiisilamu yaani Madrasa huku wakiendeleza yale ya mfumo wa kawaida wa elimu nchini Tanzania.

Also Read
Shishi Baby Vs Vanessa Mdee

Binti yake mkubwa ambaye anasubiri kujiunga na kidato cha tano anasoma kozi fupi ya “Computer” na Shishi alisema mtoto huyo hupelekwa chuoni na dereva asubuhi na kurejeshwa nyumbani baada ya masomo ili kumlinda kutokana na watu ambao wanaweza kutaka kuingilia maisha ya mwanawe ili kumuumiza yeye.

Also Read
Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Shishi ambaye hukiri wazi kwamba hakupata nafasi ya kupata elimu anaonekana kuwa bora kama mama mlezi ikilinganishwa na muigizaji Frida Kajala ambaye maajuzi alizomewa na wengi nchini Tanzania kwa jinsi analea mtoto wake kwa jina Paula.

Paula alionekana kwenye video na msanii Rayvanny wakibusiana jambo ambalo mwishowe lilisababisha msanii huyo akamatwe na polisi na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.

  

Latest posts

Zuchu Amtania Mamake Khadija Kopa

Marion Bosire

Muigizaji Jaymo Afunga Ndoa

Marion Bosire

Don Jazzy Anatafuta Kumsajili Salle

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi