Sofiane Bakali awasili Nairobi tayari kushiriki Kip Keino Classic

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji Sofiane El Bakkali wa Moroko ndiye mwanariadha w akwanza kuwasili jijini Nairobi kushiriki makala ya pili ya mashindano ya Kip Keino Classic Continental tour Jumamosi ijayo Septemba 18 katika uwanja wa Kasarani.

Also Read
Anthony Joshua kuzichapa dhidi ya Kubrat Pulev Desemba 12

Bakkali amewasili mapema Jumamosi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akiandamana na mkalimani wake.

Soufiane Bakkali  akiwa na mkalimani wake katika  uwanja wa JKIA

“Hii ni mara yangu ya kwanza kuzuru Kenya na ninatarajia kufanya vyema yakiwa pia ni mashindano yangu ya mwisho mwaka huu” akasema Bakkali

Also Read
Seminaa kuhusu ulaji muku kwa wanariadha mjini Kapsabet yahaarishwa hadi Machi 9

Bakkali alizima ukiritimba wa Wakenya kwenye michezo ya Olimpiki mwaka huu aliponyakua dhahabu katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji tangu mwaka 1968.

Also Read
Peres Jepchirchir alenga taji ya Valencia marathon

Mwanariadha huyo kutoka Moroko,Christine Mboma kutoka Namibia  ni miongoni mwa wanariadha tajika  watakaoshiriki mashindano hayo.

Mkondo wa Kenya utakuwa wa 12 na wa mwisho wa mashindano ya Continental tour nembo ya dhahabu huku yakiandaliwa kwa mara ya pili nchini.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi