Soko jipya la mavazi ya mitindo ya vipusa kufunguliwa

Soko jipya la mavazi ya mitindo ya wanawake maarufu kama DadaSoko litafunguliwa jijini Nairobi Jumamosi hii , katika klabu cha burudani cha K1 eneo la Parklands.

 

Soko hilo jipya ambalo pia litakuwa linapatikana kupitia mitandaoni na linafuatia kufunguliwa kwa jingine nchini Marekani , eneo la Waldorf Astoria Las Vegas mapema mwezi huu .

Mapambo pamoja na mavazi ya kila aina ya wanawake, yatakuwa yakiuzwa katika soko hilo na ni mradi ulioanzishwa na kundi laa wanawake wajasiriamali.

Also Read
Usajili wa mashirika matatu ya wanamuziki watupiliwa mbali

Kulingana na Rais na mwanzilishi mwenza wa soko hilo Moses Kusasira lengo lao ni kuwawezesha kupitia kwa biashara ya mitandaoni .

“Huu ni mradi wa kijamii usio wa faida ambao unajisimamia . Sokodada ni soka la kibiashara la mtandaoni ambalo ni mahususi kwa akina dada wajasiriamali  barani Afrika , linalolenga kuwawezesha  kupitia kwa biashara kwa   njia za kidijitali”akasema Kusasira

Also Read
Vampino Sasa Yuko Huru

Wasanii  wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi huo ni pamoja na  Fena Gitu Sanaipei Tande,  na kundi la Ma Dj wanawake wakiongozwa na   Sheila Mwanyigha

“Tangu Septemba  mradi wa DadaSoko umekuwa ukitoa mafunzo kwa mamia ya wafanyi biashara wanawake  kutoka mijini na mashinani  kote nchini Kenya.

Wote wanaohitimu hupewa fursa ya kumiliki maduka kupitia mtandao wa DadaSoko  kuuza bidhaa na huduma  zao  “akasema  Peter Munyasia mkurugenzi mwanzilishi  wa mradi wa global soko na pia mwanzilishi mwenza wa DadaSoko.

Also Read
"Jifunzeni kwangu na Ali Kiba." Diamond Platnumz

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya  Nairobi Esther Pasaris ametaja  soko hilo kuwa mwamko mpya kwa akina dada.

“Njia pekee ya kusaidia vijana ni kubuni  miradi ya kutega uchumi kama hii ambayo itawapa fursa ya kudhihirisha  uwezo wao sio tu  nchini bali hata kimataifa”akakariri Pasaris

  

Latest posts

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Akothee Atangaza Ziara

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi