Solanje Knowles asema alikuwa akiugua huku akitayarisha muziki

Mwanamuziki wa Marekani Solanje Knowles ambaye ni dadake Beyonce anasherehekea miaka miwili tangu kuachia kazi yake ya muziki iitwayo, “When I get Home”.

Kwenye harakati hizo, mwanamuziki huyo amefichua kwamba wakati alikuwa akitayarisha kazi hiyo alikuwa akiugua na hakudhania kwamba angeishi kwa muda mrefu.

Anasema wakati huo alikuwa analazwa hospitalini mara nyingi na wakati mmoja aliuliza Mungu amwonyeshe ikiwa ni mwisho wake na aikiwa angepona basi angesonga na kuendeleza kazi yake vilivyo.

Also Read
Chloe X Halle watangazwa mabalozi wa bidhaa za Neutrogena

Solange hajasema alikuwa akiugua nini lakini mwaka 2017 alilazimika kutangaza kwamba alikuwa na tatizo la neva ambazo hudhibiti vitendo visivyodhibitiwa na akili ya mtu baada ya kukosa kuhudhuria tamasha nchini Afrika Kusini.

Mwanamuziki huyo ambaye anatoka kwenye familia ya wanamuziki, alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo pale ambapo alikuwa anasaidia kundi la “Destiny Child” ambalo dadake mkubwa alikuwa mwanachama.

Also Read
Ujauzito wa Amber Rutty waharibika

Akiwa na umri wa miaka 16 (mwaka 2002) Solanje alizindua albamu yake yakwanza kwa jina “Solo Star” baada ya kujisajili kwenye kampuni ya babake iitwayo “Music world Entertainment”.

Baada ya hapo aliingilia uigizaji na kuandikia wanamuziki wengine nyimbo kazi ambayo ilidumu kati ya mwaka 2005 na 2007.

Dada huyo mdogo wa Beyonce ambaye ana umri wa miaka 34 sasa amewahi kuolewa mara mbili. Mara ya kwanza mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 17 tu alifunga ndoa na Daniel Smith ambaye alikuwa na umri wa miaka 19 na walibarikiwa na mtoto mvulana naye mwaka huo mwezi Oktoba. Ndoa yao ilisambaratika mwaka 2007.

Also Read
Stephanie Okereke Linus ateuliwa balozi wa usafi wa mazingira Nigeria.

Mara ya pili aliolewa na Alan Ferguson mwaka 2014 hadi 2019.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi