Somalia yafungua tena ubalozi wake Jijini Nairobi

Somalia imefungua upya ubalozi wake jijini Nairobi baada ya takriban miongo mitatu.

Akiongea alipoongoza hafla ya kufungua upya ubalozi huo, Katibu Mkuu Mwandamizi wa Wizara ya Mashauri ya nchi za kigeni Ababu Namwamba amesema kufunguliwa upya kwa ubalozi huo ni hatua muhimu katika juhudi za kujenga upya nchi ya Somalia.

Also Read
NEMA yasimamisha mradi wa Mzuri Sweets wa mabilioni ya pesa huko Kilifi

Namwamba amesema Kenya itaendeleza juhudi zake za kufanikisha amani, udhabiti na ufanisi nchini Somalia na eneo zima la upembe wa Afrika.

Aidha ametoa hakikisho kuwa Kenya imejitolea kuimarisha zaidi uhusiano wa pande mbili kati ya nchi hizi mbili na pia kutetea masuala ya Somalia na bara hili kwa jumla kwenye mikutano ya kimataifa wakati huu wa enzi yake kama mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2021 na 2022.

Also Read
Visa 796 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

“Azimio letu la pamoja kwa ajili ya amani ya kudumu, iliyo imara na maendeleo endelevu kwa ajili ya wananchi wa mataifa yote mawili na eneo zima linaendelea kudhihirisha umuhimu wa ushirikiano wetu,” Amesema Namwamba

Also Read
Msiwafukuze wanafunzi kwa sababu ya karo, aonya Prof Magoha

Jengo la sasa lililo karibu na barabara ya Lower Kabete lilinunuliwa na serikali ya Somalia mwaka wa 1972 na halijatumika tangu mwaka wa 1994 wakati Somalia lilipokumbwa na machafuko.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi