Somalia yahimiza Kenya kufungua ubalozi wake nchini humo

Somalia imeihimiza Kenya ifungue ubalozi wake nchini humo kufuatia kuboreshwa kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Somalia ilisema itafungua ubalozi wake hapa Kenya.

Kwenye taarifa, Waziri Mkuu wa Somalia alisema kurejelewa kwa shughuli za kidiplomasia itakuwa fursa bora ya kuanzisha mashauriano kuhusu mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Also Read
Nancy Chelangat afuzu kwa fainali ta mita 1500 T11 huku Waithera Njoroge na Nelly Munialo wakiambulia sakafu Olimpiki ya walemavu Tokyo

Haya yanajiri huku Somalia wiki iliyopita ikikaribisha hatua ya Kenya ya kuondoa marufuku ya safari za ndege kuingia na kutoka nchini humo.

Also Read
Malkia Striker wapoteza mechi ya tatu mtawalia dhidi ya mabingwa wa dunia Serbia katika Olimpiki

Siku ya Alhamisi, Kenya kupitia Wizara ya Mashauri ya nchi za kigeni ilisema kwamba imebadili uamuzi wake wa awali kutokana na maslahi ya pande zote mbili, ikitumai kwamba mahusiano kamili ya nchi hizo mbili yatarejelewa.

Also Read
Kenya yaibwaga Ethiopia Cecafa

Kenya ilisitisha safari za ndege za kutoka Somalia kwa takriban mwezi mmoja baada ya uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kudorora.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi