Somalia yamkataa John Mahama kuwa mpatanishi wa mzozo kati yake na Kenya

Somalia imemkataa mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika (AU) ambaye aliteuliwa kuwa mpatanishi kwenye mazungumzo kuhusu mzozo wa kisiasa baina ya taifa hilo na Kenya.

AU ilikuwa imemteua Rais wa zamani wa Ghana John Mahama kuwa mpatanishi kati ya nchi hizo mbili.

Also Read
Refa wa Libya Mutaz Ibrahim kusimamia mchuano wa Kenya na Comoros

Kwenye barua kwa tume ya muungano wa Afrika, Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Somalia Moussa Faki Mahamat alisema kwamba Mahama ana uhusiano mkubwa na Kenya na hivyo hatakubaliana naye katika jukumu lake kama mpatanishi.

Barua hiyo iligusia umuhimu wa jukumu kama hilo na kuongeza kwamba ni muhimu kwa mpatanishi kama huyo kuwa asiyependelea upande wowote, na asiye na uhusiano wowote na kanda hii ya Afrika.

Also Read
Kenya kubuni kamati ya kusuluhisha mzozo wa kidiplomasia na Somalia

Aidha, Somalia ilisema uamuzi wa kumteuwa mjumbe maalum umepitwa na wakati, kwani Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hussein Roble tayari ameafikia makubaliano kuhusu hatua ya pande hizo kurejelea mazungumzo.

Also Read
Senegal ya kwanza kufuzu AFCON 2022

Hivi majuzi Somalia iliishtumu Kenya kwa kuingilia siasa zake za ndani, kabla ya uchaguzi ambao kwa sasa umeahirishwa.

Hata hivyo Kenya imekanusha madai hayo.

  

Latest posts

Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Tom Mathinji

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai nchini Tanzania afungwa miaka 30 gerezani

Tom Mathinji

Mbunge Sir David Amess auawa kwa kudungwa kisu nchini Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi