Spika wa Bunge la Kaunti ya Migori na Naibu wake wakamatwa kwa madai ya ufisadi

Maafisa kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC, wamemkamata Spika wa Bunge la Kaunti ya Migori Boaz Okoth na Naibu wake Mathews Chacha.

Wawili hao wamekamatwa pamoja na maafisa kadhaa wa bunge hilo kwa madai ya kuhusika kwenye kesi ya ufisadi ambayo imekuwa ikichunguzwa na maafisa wa EACC.

Also Read
ODM yaunga mkono kubanduliwa kwa Gavana wa Migori Okoth Obado

Karani wa bunge hilo Tom Opere, naibu wake Emmanuel Aballa Kingwara na Mkuu wa Kitengo cha Uagizaji bidhaa na huduma Steve Okello ni miongoni mwa wale waliokamatwa.

Also Read
EACC yamezea mate mali ya aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu

Kwenye barua ya tarehe tano mwezi Novemba mwaka huu, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma iliidhinisha kukamatwa kwa washukiwa hao kwa madai ya ufisadi.

Spika Boaz Okoth alichukua msimamo mkali wakati wa jaribio la kubanduliwa kwa Gavana wa Kaunti hiyo Okoth Obado ambaye pia anakabiliwa na kesi ya ufisadi.

Also Read
Rais Kenyatta aongoza mazungumzo kati ya wajumbe wa Kenya na wa Somaliland

Mswaada wa kubanduliwa kwa Obado ulikosa kujadiliwa huku baadhi ya wanachama wa bunge hilo wakizusha vurugu.

Ni kipindi hicho cha mswaada huo ambapo Naibu Spika Chacha aliapishwa.

  

Latest posts

Kenchic yazindua aina tatu mpya ya bidhaa za kuku

DOtuke

Munya: Covid-19,Nzige na ukame, Chanzo cha gharama ya juu ya maisha

Tom Mathinji

Kenya yaadhimisha wiki ya kimataifa ya kuwanyonyesha watoto

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi