Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Kampuni ya mchezo wa kamari ya Sportpesa imetangaza kurejesha ufadhili wake kwenye michezo humu nchini baada ya kusitishwa kwa muda.

Akitangaza hayo CEO wa kampuni hiyo Ronald Karauri,  amesema kuwa kampuni hiyo imeinuka tena baada ya kupitia changamoto ambazo almanusra zisababishe kufunga biashara.

Ceo wa Sportpesa Ronald Karauri

“Tumerejea baada ya kupitia wakati mgumu na sasa tutawekeza katika michezoni nchini sawa na ilivyokuwa awali,sio tu katika mchezo wa ngumi , bali tutakuwa tukijihusisha na michezo mingi humu nchini kama ilivyokuwa awali”akasema Karauri

Also Read
Wakenya kushuka ulingoni siku ya tatu ya Africa Zone 3

Karauri alisema haya alipoongoza kufungua ukumbi wa ngumi katika mtaaa wa umoja ambao uliezekwa paa na kampuni ya Sportpesa kwa kima cha shilingi milioni 1 nukta 2.

Mbunge wa Embakasi  West  George Theuri

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la mchezo wa ngumi nchini Athony Ombok almaarufu Jamal ambaye pia alihudhuria hafla hiyo ,amewaomba wahisani kujitokeza na kupiga jeki mchezo huo.

Also Read
Hit Squad yaanza mazoezi kwa mashindano ya dunia nchini Serbia mwezi Oktoba
Rais wa shirikisho la ngumi BKF Antony Jamal

“Imekuwa vigumu kuendesha mchezo kwa kutumia hela za mfuko,naomba kama kuna wahisani ,makampuni wanaoweza kujitokeza ili kufadhili mchezo huo,tumefanya mengi hadi sasa katika ukuzaji wa mchezo ikiwemo mradi wa ndondi mashinani na inaonyesha mchezo umekuwa na ikiwa tutapata wahisani tutafanya makubwa” akasema Jamal

Bondia Fatuma Zarika ambaye ni mshindi wa zamani wa mkanda wa wbc amefurahia ukumbi huo ambapo amekuwa akifanyia mazoezi tangu akiwa mtoto na kuongeza kuwa utakuza vipaji vingi mtaani Umoja na viunga vyake.

Also Read
Mashindano ya msururu wa dunia katika raga ya wachezaji 7 upande HSBC kuanza Mei
Fatuma Zarika

“Hii ni kitu imenifurahisha sana kuona hii dream imekuwa reality najua sasa vijana wengi watanufaika na huu ukumbi,niishukuru Sportpesa sana kwa  mradi huu”akasema Zarika

Ukumbi huo una uwezo wa kumudu mabondia 30 kwa wakati mmoja wakifanya mazoezi na ulifanyiwa ukarabatio maajuzi.

  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi