Tume ya mishahara na marupurupu-SRC imeidhinisha mikopo ya kununulia magari kwa wawakilishi wa Wadi na maspika wa bunge za kaunti.
Mwenyekiti wa tume hiyo Lyn Kimengich,kwenye waraka kwa mwenyekiti wa baraza la magavana Martin Wambora alisema serikali za kaunti zitapewa utaratibu kuhusu utekelezaji wake.
Haya yanajiri baada ya Wambora kuiandikia barua tume hiyo akitaka wawakilishi wa wadi kupewa mikopo hiyo kama wanavyopewa wabunge.
Tume hiyo ilikubali kugeuza mikopo hiyo kuwa ruzuku,huku ikisema haitagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.5 zilizoidhinishwaa
Hata hivyo manufaa hayo yanawahusu tu maspika wa sasa na wawakilishi wa Wadi.
Tume hiyo imesema ni vyema wawakilishi hao kufurahia marupurupu hayo kama wabunge.
Aidha tume hiyo ilisema ilikuwa imetoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo.