SRC yaondoa marupurupu ya kuhudhuria vikao vya bunge

Na Agnes Mwangangi.

Tume ya kuratibu mishahara na marupu rupu humu nchini –(SRC), imeondolea mbali marupurupu ya kuhudhuria vikao vya bunge la 13, na hivyo kui-okolea serikali shilingi million 382.2.

Bunge la kitaifa lina wabumbe 349 huku lile la Seneti likiwa na wajumbe 67, ambapo kila mmoja wao hupokea marupu-rupu ya kuhudhuria vikao vya bunge ya shilingi elfu-5 kwa kila kikao.

Also Read
Muturi awataka wanataaluma kusaidia jamii kuboresha Maisha

Bunge la kitaifa huandaa vikao vyake mara nne kwa wiki, huku lile la seneti likiandaa vikao vitatu kwa wiki.

Wabunge walifahamishwa kuhusu uamuzi huo wakati wa kikao kati yao na Spika siku ya Jumatano.

Hata hivyo wabunge hao 416 watafurahia masharti nafuu ya mikopo ya kununua magari ya hadi shilingi million 10 kila baada ya miaka mitano, ambapo watahitajika kununua gari la engine isiyozidi Cubic Lita 3,000 za mafuta.

Also Read
SRC yaidhinisha ruzuku ya kuwanunulia gari wawakilishi wadi

Hata hivyo marupu-rupu ya kuhudhuria vikao vya kamati za bunge ya shilling 15,000  kwa mwenyekiti, shilling 10,000 kwa naibu mwenyekiti na shilling 8,000 kwa mwanachama wa kawaida yamedumishwa.

Also Read
Rais Kenyatta awateua watu watano kujiunga na TSC

Spika wa Bunge la kitaifa Justin Muturi hata hivyo ameshtumu hatua ya tume hiyo.

Kulingana na Spika Muturi, tume ya  SRC haingepaswa kuchukua hatua hiyo, ikizingatiwa kuwa wabunge wa mataifa jirani wanapokea marupurupu hayo ya kuhudhuria vikao vya bunge.

  

Latest posts

Serikali ya Uingereza yaidhinisha uuzaji wa klabu ya Chelsea kwa pauni bilioni 4 nukta 25

Dismas Otuke

Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Tom Mathinji

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi