Star Times wasaini mkataba wa miaka 7 na FKF kwa kima cha milioni 836

Kampuni ya Uchina  Star Times imesaini mkataba wa miaka 7 kupeperusha mbashara  mechi zote za   timu za taifa Harambee Stars, Harambee starlets na ligi kuu ya Fkf ,na mechi 30 za  ligi ya kitaifa Supa (Nsl).

Also Read
Uganda Cranes waendelea na mazoezi katika uwanja wa Utalii kujiandaa kwa mchuano wa Septemba 2 dhidi ya Kenya

Mkataba huo ni wa kima cha shilingi milioni 836 ,ikiwa dola milioni 1 nukta 1 kwa mwaka  huku mchuano wa kwanza kupeperushwa ukiwa ule wa kirafiki baina ya Kenya na Zambia  Tarehe 10 mwezi huu.

Soka ya Kenya haijakuwa na mdhamini wa runinga tangu kung’atuka kwa Super sport mwaka 2017 baada ya kuhudumu kwa miaka 10 ambapo walikuwa wakitoa ufadhili wa shilingi milioni 380 kwa mwaka .

Also Read
Kenya yaanza mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya CECAFA

Mkataba huo unatarajiwa kusainiwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ,pengine mwezi ujao na unaleta matumaini katika soka ya Kenya  baada ya ufadhili wa shilingi bilioni 1 nukta 2 kutoka kwa kampuni ya Betking kufadhili ligi kuu ya Kenya.

Also Read
Mashabiki wapigwa marufuku Olimpiki

 

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi