Stars yaendeleza mazoezi kujiandaa kukabiliana na Misri na Togo

Timu ya taifa Harambee Stars inaendelea na mazoezi kujiandaa kwa mechi za kirafiki na pia michunao ya kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika AFCON mwaka ujao nchini Cameroon.

Stars watachuana na Sudan Kusini tarehe 13 mwezi huu katika mechi ya kwanza ya kirafiki kabla ya kuialika Tanzania Machi 15 na baadae kuzuru Tanzania kwa mechi ya marudio tarehe 18.

Also Read
Morans na Shujaa kuvaana semi fainali ya Safari 7's

Kenya itawaalika Pharoes ya Misri katika mechi ya 5 ya kundi F kufuzu kwa dimba la AFCON kabla ya kuzuru Lome Togo Machi 30 kwa mechi ya mwisho.

Also Read
Tanzania wakwea ndege kupiga kipute cha AFCON mwakani

Wachezaji wanaopiga soka humu nchini waliripoti kambini Februari 28, kabla ya kuanza mazoezi Machi 1.

Kwa mjibu wa kocha wa Stars Jacob Mulee atatumia mechi hizo mbili dhidi ya Misri na Togo kama maandalizi ya mechi za makundi kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazoanza Juni mwaka huu.

Also Read
Tusker FC waleweshwa mara nne na Zamelek na kutemwa nje ya ligi ya mabingwa

Kenya imo kundi moja la kufuzu pamoja na mibabe Mali,majirani Uganda na Rwanda.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi