StarTimes yakatiza mkataba wa shilingi milioni 110 kwa mwaka na na FKF

Kampuni ya runinga ya Uchina ,StarsTimes imekatiza mkataba wa miaka 7 wa matangazo ya soka ya Kenya kupitia runinga .

Mkataba huo wa miaka 7 ulikuwa wa kima cha  shilingi milioni 110 kwa kila mwaka ambacho ndicho kiwango cha pesa StarTimes imekuwa ikilipa FKF.

Kwenye barua yake StarTimes imetaja sababu za kutamatisha mkataba huo kama ukiukaji wa mwafaka baina yao na shirikisho la kandanda nchini FKF waliosaini Septemba 29 mwaka 2019.

Also Read
Vihiga Queens Fc walenga kuanza vyema ligi ya mabingwa
Startimes wakisaini mkataba na FKF

Kampuni hiyo imelalama kuwa licha ya kutekeleza sehemu ya mkataba ikiwemo kulipa pesa kwa wakati ufaao,FKF hawakuwajibika kikamilifu ikiwemo kukosa kuwasilisha mechi kadhaa zilizohitajika ili zipeperushwe hususan mechi ya ligi kuu baina ya AFC Leopards na Gor Mahia maarufu kama Mashemeji Derby .

 

Pia FKF ilikuwa ikibadilisha ratiba ghafla ,mvutano kati FKF na vyombo vya habari na klabu kuu ambayo imeathiri biashara yao shirikisho kukosa kutimiza malengo yake ya kila wiki ikiwemo kupeperusha mchuano mmoja bila malipo kwa mashabiki ,kipindi cha kila wiki cha ligi kuu na kukosa kukiri Star times kuwa wamiliki wa haki za matangazo ya runinga ya ligi ya Kenya.

Also Read
Wanamichezo 11 wapokea msaada wa masomo kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini NOCK

Hata hivyo StarTimes imekariri kuwa inanuia kurejea kufadhili soka ya Kenya siku zijazo na wako tayari kusaini mkataba ambao hautahatarisha biashara yao .

Also Read
Olunga atawazwa mfungaji bora ligi kuu Japan kwa kupiga bao la 27

Kujiondoa kwa StarTimes kunajiri ,miezi michache baada ya wafadhili wakuu wa ligi ya Kenya Betking kujiondoa kwa hali ya kutatanisha huku masaibu yakizi kumzonga aliyekuwa kinara wa FKF Nick Mwendwa aliyeng’atuliwa mamlakani na waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed aliyeunda kamati ya muda kuendesha soka ya Kenya .

  

Latest posts

Kombe la dunia kuwasilishwa nchini wiki ijayo

Dismas Otuke

Wanamichezo 11 wapokea msaada wa masomo kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini NOCK

Dismas Otuke

Kenya Pipeline waelekea Tunisia kwa mashindano ya klabu bingwa kwa vidosho

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi