Sudan yafuzu kwa kipute cha AFCON baada ya subira ya miaka 9

Sudan ilijikatia tiketi kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Cameroon kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 walipoilaza Bafana Bafana ya Afrika Kusini mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya kundi C iliyosakatwa Jumapili jioni uwanjani Al Hilal Stadium mjini Omdurman .

Sudan maarufu kama The Falcons of Jediane walimaliza kibarua katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mabao ya Saifeldin Maki na Mohamed Abdel Rahman na kujihakikishia tiketi ya AFCON Kwa mara ya 9 huku Afrika Kusini ikikosa .

Also Read
Mashindano ya riadha yahamishwa kutoka Bondo hadi Nairobi

Sudan walicheza fainali za AFCON kwa mara ya mwisho mwaka 2012 wakibanduliwa katika robo fainali na wamefuzu mwaka huu baada ya kuibuka wa pili katika kundi C kwa alama 12 ,moja nyuma ya Afrika Kusini huku Afrika Kusini ikiibuka ya tatu kwa alama 10.

Also Read
Samatta ajiunga na Fernabache ya Uturuki kwa mkopo mrefu

Mataifa 18 yamefuzu kwenda AFCON ya Cameroon mwaka ujao huku nafasi 6 zilizosalia zikijazwa baina ya Jumatatu na Jumanne wakati wa kukamilika kwa mechi za makundi .

Timu 18 zilizotinga AFCON ni pamoja Mali na Guinea kutoka kundi A,Burkina Faso ya kundi B,Ghana na Sudan za kundi C,Gabon na Gambia kutoka kundi D,Moroko kutoka kundi E,Cameroon kutoka kundi F,Misri na Comoros za kundi G,Algeria na Zimbabwe kutoka kundi H,Senegal ya kundi I,Tunisia na Equitorial Guinea za kundi J,Ivory Coast ya kundi K pamoja na Nigeria kutoka kundi L.

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi