Sukari ya Chemilil yakosa ‘utamu’ baada ya kuvunjwa kwa kilabu cha Chemilil Sugar FC

Timu ya Chemilil Sugar FC  iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya Kenya KPL ,imevunjiliwa mbali huku wachezaji na maafisa wote wa benchi la kiufundi wakiruhusiwa kuondoka.

Chemilil FC  ilivunjwa Jumanne jioni ikiwa miezi michache tangu washushwe daraja kutoka ligi kuu  walikocheza kwa miaka  24 bila kuteremshwa ngazi.

Kulingana na mwenyekiti wa timu hiyo Collins Agayi wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya serikali kutangaza kukodisha viwanda vyote vya sukari vya Chemilil  na pia kutoa arifa Julai 6 mwaka huu ya kusitisha shughuli zote za kuajiri ,kupandisha vyeo na majukumu mengine ya kimataifa kwa wafanyikazi wote wa kampuni  ya kusaga miwa ya Chemilil inayokumbwa na masaibu chungu tele ya kifedha .

Also Read
Batoto Ba Mungu kuzindua uhasama na Tusker FC ligi kuu Ijumaa
Kikosi cha Chemilil Sugar Fc msimu jana kabla ya  mojawapo ya mechi ya  ligi kuu KPL

Timu hiyo iliyoshushwa ngazi msimu jana ilitarajiwa kushiriki ligi kuu  ya daraja ya kwanza  NSL  msimu mpya utakapoanza ,Tarehe 28 mwezi huu

Also Read
Kocha wa Gor Mahia Andreas Spier afunganya virago

Yamkini timu hiyo inadaiwa malimbikizi ya mishahara ya wachezaji  huku baadhi  yao wakitaka walipwe pesa zao hususan kufuatia kuvunjwa kwa timu.

Chemilil Sugar Fc  imekuwa miongoni mwa vilabu vnavyofadhiliwa na mashrika katika ligi kuu ya kenya lakini masaibu yao yalianza wakati kampuni ya Chemilil Sugar ilianza kudorora kifedha.

Sony Sugar Fc pia iliteremshwa ngazi kutoka ligi kuu ya KPL baada ya kushindwa kusafiri kucheza mechi tatu wakati wenzao Nzoia Sugar pia wakikosa mchuano mmoja wa ugenini katika ligi kutokana na uhaba wa pesa.
  

Latest posts

Manara na Hersi Matatani

Marion Bosire

Mary Moraa Bingwa wa Mita 800 kwa Wanawake Kwenye Michezo ya Jumuia ya Madola Mwaka 2022

Marion Bosire

Chebet na Jebitok wafuzu fainali ya mita 1500 michezo ya jumuiya ya madola

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi